Maji Week 2020

Siku ya Maji

Wizara ya Maji imekuwa ikiratibu Wiki ya maji kitaifa kila mwaka hapa nchini kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya maji. Maadhimisho haya yanatokana na Azimio Na. 47/193 la Umoja wa Mataifa (UN) kuwa kila ifikapo Machi, 22 ya kila mwaka nchi wanachama ziadhimishe siku ya maji Duniani kwa pamoja.

Hii ni Katika kutambua umuhimu na thamani ya maji katika maisha ya binadamu na uchumi wa Dunia kwa ujumla

Lengo kuu la maadhimisho ya Wiki ya Maji nchini ni kuungana na Mataifa mengine katika kutathimni utekelezaji, mafanikio, changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maji na kuainisha mikakati ya kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira na kusimamia utunzaji wa rasilimali ya maji nchini.

Taarifa kwa Umma: Kusitisha Shughuli Kuelekea Siku ya Maji Duniani

Taarifa kwa vyombo vya Habari: Wiki ya Maji

2020 Maji (Water) Week Registration: Register before 20 February, 2020: click this link

Second call for Abstracts/Call for Sessions: 2020 Maji (Water) Week Annual Scientific Conference


Maji Week Exhibition: Dar es salaam, Click this link for details