Majukumu ya Msingi

Majukumu makuu ya Wizara ya Maji

Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa Sera, Mikakati na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji.

Kutayarisha na kusimamia sheria, kanuni na taaratibu zinazosimamia Sekta ya Maji;

Kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji;

Kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kuhifadhi takwimu muhimu za Sekta ya Maji;

Kutoa miongozo ya kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za maji;

Kutoa miongozo ya utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira vijijini na mijini;

Kutoa mafunzo kwa Wataalam wa Sekta ya Maji katika ngazi na kada mbalimbali za utekelezaji;

Kuendeleza tafiti kuhusu teknolojia bora zinazotumika katika kutoa huduma ya maji;

Kuratibu majukumu na kutekeleza ushauri wa Bodi ya Taifa ya Maji