Habari

Imewekwa: Dec, 03 2023

Waziri Aweso awaongoza wadau kujadili upatikanaji fedha ujenzi bwawa la Songwe

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Songwecom ameongoza mkutano wa wadau, viongozi, Wizara za Kisekta na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) kuhusu upatikanaji wa fedha za ujenzi wa bwawa la Songwe.

Pamoja naye, mkutano huo uliojadili suala la upatikanaji wa fedha umemshirikisha Mwenyekiti Mwenza wa Songwecom, Waziri wa Maji wa Malawi Mhe. Abida Sidik Mia.


Mradi wa ujenzi wa bwawa la Songwe unahusu nchi za Tanzania na Malawi na moja ya malengo yake ni kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwamo kuzuia mafuriko, upatikanaji wa maji, uzalishaji wa nishati ya umeme, kilimo cha umwagiliaji, uvuvi na maji ya mifugo.


Mkutano huo umehudhuriwa na Wizara za kisekta zinazotarajia kunufaika na kwa upande wa Tanzania ikiwamo Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo, na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.