Habari

Imewekwa: Dec, 08 2023

​TAARIFA KWA UMMA - UTEUZI

News Images

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) leo tarehe 08 Desemba, 2023 amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao;

  • 1.Mhandisi Abbas Pyarali kuwa Mkurugenzi Msaidizi, Usanifu na Usimamizi wa Miradi ya Maji Wizara ya Maji, awali alikuwa Mhandisi Mkuu katika Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira, Wizara ya Maji.
  • 2.Mhandisi Ndele Mengo kuwa Mkurugenzi, Sehemu ya Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa, ambaye awali alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi RUWASA (taratibu za kiofisi kufanya eneo hili kuwa wakala zinaendelea).
  • 3.na Mhandisi Mariam Majala kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Ufundi, RUWASA ambayealikuwa Meneja wa RUWASA mkoa wa Simiyu.
  • Waziri Aweso amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyonayo kupitia Sheria Namba 5 ya Mwaka 2019 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira
  • Kitengo cha Mawasiliano