Habari
Waziri Aweso Atoa Siku 14 DUWASA Kukamilisha Mradi Wa Maji Nala, Akagua Uchimbaji Visima Nkuhungu

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) ametembelea na kukagua ujenzi wa miradi ya majisafi katika Kata ya Nala na Nkuhungu mkoani Dodoma ili kuona maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo.
Katika ziara hiyo Waziri Aweso ameambatana na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini ambaye pia ni Waziri wa Madini Mhe Anthony Mavunde.
Mhe Aweso ametoa wiki mbili kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingiria Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph kukamilisha mradi wa Nala ili wananchi waanze kupata huduma.
Mradi huo unatekekezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 3.83 kwa awamu mbili.
Awamu ya kwanza utanufaisha wakazi
zaidi ya elfu tano wa Nala Centre, Segu Juu na Chihoni ndani ya Kata ya Nala pamoja na kiwanda cha mbolea cha Nala – Itracom.
Awamu ya pili ya mradi itaongeza upatikanaji wa maji kwa wakazi zaidi ya elfu nane.