Habari
Katibu Mkuu Maji aongoza kikao kuhusu maendeleo ya Bwawa la Farkwa
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri ameongoza kikao cha Kamati ya Uongozi (steering committee) ya Bwawa la Farkwa ili kujadili maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Bwawa hilo.
Bwawa la Farkwa linajengwa katika Kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoa wa Dodoma likilenga kuwezesha huduma ya majisafi na salama katika Jiji la Dodoma na miji ya Chamwino na Bahi. Wakazi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mradi tayari wamelipwa fidia ili kupisha mradi huo.
Mhandisi Mwajuma ameiagiza Kamati hiyo kuhakikisha inaondoa changamoto zote zinazoweza kukwamisha utekelezaji wa mradi huo. Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatambua changamoto wanayopitia wananchi wa jiji la Dodoma na miji ya Bahi na Chamwimo hivyo ameagiza kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa ili huduma ya majisafi iwafikie haraka.