Wasifu

Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Ununuzi
Raphael Mahundi
Bw. Raphael Mahundi alihamishiwa Wizara ya Maji mwezi Mei, 2024 . Kabla ya hapo alikuwa Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mkufunzi wa masomo yanayohusu taratibu za kuanzisha miradi, kuwapata watoa huduma za ujenzi ikiwa ni pamoja na Wakandarasi na Wahandisi Washauri Elekezi; na kusimamia miradi ya ujenzi.
Bw. Mahundi ana Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Miradi ya Ujenzi (MSc. Construction Management) kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyoipata mwaka 2014. Ni mmbobezi katika majukumu mbalimbali yanayohusu ununuzi wa umma, kama vile kufanya ukaguzi wa manunuzi, kuandaa nyaraka za kufundishia na kufundisha juu Sheria ya Ununuzi wa Umma. Pia amepata nafasi ya kuandaa nyaraka mbalimbali za ununuzi (Tender Documents) za miradi ya ujenzi hususani miradi ya maji.