Wasifu

Abeid G. Kiangi

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Huduma za Ubora wa Maji, Sehemu ya ushauri wa Kitaalamu

Abeid G. Kiangi

Abeid Gladson Kiangi anasimamia miongozo ya usimamizi wa shughuli za tafiti za ndani zinazohusu masuala ya ubora wa maji; anafanya kazi ya kutoa ushauri wa kitaalamu kwenye mitambo ya kusafisha maji kuhusiana na madawa yanayotumika kusafisha na kutibu maji; Kusimamia mchakato wa kupata ithibati kwa maabara za maji; Kutoa ushauri kuhusu mapitio na uboreshaji wa viwango vya ubora wa maji na majitaka. Aidha anaratibu mchakato wa ithibati za maabara za maji na mipango ya uhakiki wa ubora wa shughuli za kimaabara.

Bwana Abeid Gladson Kiangi ana shahada ya uzamili ya Sayansi ya Usimamizi wa Mazingira [Master of science in Environmental Studies (Management)]; Pia ana Shahada ya Sayansi katika fani ya Kemia na Zoolojia.

Kabla ya kuteuliwa kwake, alikuwa Meneja wa Maabara Kuu ya Ubora wa Maji ya Dar es Salaam na kabla ya hapo alifanya kazi kama mtaalamu wa ubora wa maji katika Maabara ya Ubora wa Maji ya Mkoa wa Ruvuma.