Wasifu

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Udhibiti Ubora na viwango vya Maji
Monica Mushi
Aliteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Udhibiti, Ubora na viwango vya Maji akiwa na jukumu la kufuatilia masuala ya ubora na viwango vya maji. Kabla ya kuteuliwa, amefanya kazi katika Maabara ya Ubora wa Maji katika Kanda ya Mwanza kama mtaalam wa masuala ya ubora wa maji na ithibati ya maabara.
Bi. Monica Mushi ana Shahada ya Uzamili (MSc. Water Management and Governance specializing in Water Quality Management) kutoka Chuo cha UNESCO-IHE Delft nchini Uholanzi, Shahada ya Kemia (BSc (Honours) in Chemistry) kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Aidha alipata mafunzo mbalimbali ya usimamizi wa rasilimali za maji, mabadiliko ya tabia nchi, ukaguzi wa vipimo vya maabara na ithibati.
Katika utendaji wake anapenda kujifunza, kufanya kazi kwa kushirikiana, kusikiliza na kuheshimu mawazo ya wengine.