Wasifu

Erasto Ndunguru

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Tathmini na Ufuatiliaji

Erasto Ndunguru

Ndugu Erasto Ndunguru ni Mchumi anayefanya kazi zinazohusu Sera, mipango na bajeti pamoja na Ufuatiliaji na Tathimini ya miradi. Ndugu Erasto anapenda na ni mbobezi wa kuandaa maandiko ya miradi au programu, uboreshaji wa sekta na kufanya ufuatiliaji na tathmini ya miradi.

Ana Shahada ya Uzamili aliyopata kutoka Berlin University of Applied Sciences- Germany, Shahada ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe- Tanzania. Alimaliza Elimu ya Sekondari ya Juu Shule ya Wavulana Songea na Elimu ya Sekondari alihitimu Maua Seminary iliyopo Mkoa wa Kilimanjaro. Alichaguliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini mwaka 2014.