Habari

Imewekwa: May, 14 2018

WAKAZI WA CHAMWINO WALIA NA TATIZO LA MABWAWA YA UMWAGILIAJI KUJAA TOPE

News Images

Wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma wameungana na viongozi wao kumlilia Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe kuwatatulia tatizo la kujaa tope kwenye mabwawa yanayotumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji yaliyopo Buigiri na Chalinze.

Tukio hilo limetokea wakati Waziri Kamwelwe alipofanya ziara ya kukagua mabwawa hayo, baada ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa Mbunge wa Chilonwa, Joel Mwaka.

Wananchi hao wamemueleza Waziri Kamwelwe kuwa maisha yao yanategemea shughuli za kilimo cha umwagiliaji wanachokiendesha kupitia mabwawa hayo, katika kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

Kwa upande wake Mhandisi Kamwelwe amewaagiza wataalamu wa Tume ya Umwagiliaji kutafuta namna ya kudhibiti tope hilo, ili shughuli za kilimo hicho zilichoanza mwaka tangu mwaka 2005 ziweze kuendelea bila kikwazo chochote.