Habari

Imewekwa: Sep, 13 2018

Profesa Mbarawa Atembelewa na Ujumbe kutoka KfW

News Images

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa leo amekutana na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Ujerumani ya KfW kwa lengo la kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji ya Lindi, Kigoma Simiyu inayofadhiliwa na benki hiyo.

Katika mazungumzo hayo Profesa Mbarawa amesema lengo la Serikali ni kuona miradi hiyo inatekelezwa kwa haraka ili wakazi wa Lindi, Kigoma na Simiyu waweze kupata maji.

Profesa Mbarawa ameiomba KfW kufuatailia kwa karibu maendeleo ya mradi wa Lindi; ambao haridhishwi na utekelezaji wake na kusisitiza Serikali itachukua hatua stahiki, ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama kama ilivyopangwa.

Tunahitaji kuweka nguvu pia kwenye mradi wa Kigoma ili uweze kukamilika, kwa upande wangu nitahakikisha hakuna kizuizi chochote na ninatumaini mtatusaidia kwa upande wenu ili tuweze kukamilisha mradi huo.

Aidha, Profesa Mbarawa aliomba KfW kuweka msukumo kwenye utekelezaji wa mradi wa maji Simiyu, kutokana na changamoto kubwa ya huduma ya maji inayokabili mkoa huo na kuwahakikishia kuwa hakuna fedha ya miradi itakayotumika kinyume na matumizi halisi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa KfW Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika, Dkt. Klaus Muller amesema watahakikisha wanazipatia ufumbuzi changamoto zilizojitekeza kwenye miradi miradi hiyo ili iweze kukamilika na kutoa huduma kwa wananchi.

Vilevile, ameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa taratibu mbalimbali ambazo zinahusiana na utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.