Habari

Imewekwa: Jul, 03 2018

PROF. MBARAWA ATEULIWA KUWA WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI

News Images

Prof. Makame Mbarawa ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji mara baada ya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais, Dkt. John Magufuli hivi karibuni.

Prof. Mbarawa amechukua nafasi ya aliyekuwa waziri kwenye wizara hiyo, Mhandisi Isack Kamwelwe aliyeenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Mbarawa alikuwa akiiongoza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.