Habari

Imewekwa: Jul, 12 2018

Mh. Prof. Mbarawa Aitaka DUWASA Kufikia Bil. 1.8 Ndani ya Miezi Sita

News Images

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo, alipotembelea kujionea utendaji na maendeleo ya DUWASA.

‘‘Hakikisheni manapunguza upotevu wa maji, ili kuongeza makusanyo kutoka bil 1.3 kwa sasa na kufikisha 1.8 bilioni ndani ya miezi sita ijayo. Upotevu wa maji ni mkubwa na kwa kuwa maji mengi sana yanapotea bure, kama mnazalisha litamilioni 48 na asilimia 28.7 zinapotea kiasi hicho ni kikubwa sana hivyo hakikisheni mnchukua hatua kumaliza tatizo hilo.’’, alisema Prof. Mbarawa.

Amesema kuwa upotevu wa maji kwa sasa ni lita milioni 16 kwa siku ambazo ni hasara kubwa kwa mamlaka na Serikali pia, ikiashiria kuwa kuna mahali yanapotea kutokana na uchakavu wa miundombinu au inawezekana kuna watu wamejiunganishia maji kiholela bila kufuata taratibu.

Akitoa ahadi katika mara baada ya kusikiliza taarifa ya mamlaka hiyo, Prof. Mbarawa alisema Serikali itahakikisha inatenga fedha ili kuongeza vyanzo vya maji vya uhakika na kuboresha miundombinu ya maji iliyopo, ili kukidhi mahitaji ya jiji la Dodoma, ikiwemo kutafuta vyanzo mbadala kwa ajili ya jiji hilo ambapo hivi sasa idadi ya watu imeongezeka kutokana na kuwa makao makuu ya nchi.