Habari

Imewekwa: Jan, 25 2019

Naibu Waziri wa Maji akagua ujenzi wa mradi wa maji Chalinze

News Images

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amemtaka Katibu Mkuu, Wizara ya Maji kuwakutanisha wadau wote wanaohusika na mradi wa maji wa Chalinze Tarehe 29 Januari, 2019 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Aweso amesema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji wa Chalinze ambao umefika asilimia 78 ya ujenzi.

Amesema kuwa wananchi wanataka maji na sio jambo jingine na kusisitiza kwa wadau wotekukutana kupanga namna ya kumaliza mradi kwa wakati na kutatua changamoto zilizopo ili wananchi wapate huduma ya maji. Mradi huo umechelewa kwasababu, pamoja na mambo mengine, mkandarasi mkuu Serikali ilimlipa fedha lakini hakuwalipa wakandarasi wengine aliowaajiri kwa ajili ya kumsaidia baadhi ya kazi (sub contractors) hali iliyosababisha kazi kusimama.

Naibu Waziri Aweso amesema malipo ambayo yameshafanyikani asilimia 61.11 ya gharama ya mkataba ambayo ni Dola za Marekani milioni 25.1.

Awali, Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Majisadi na Maji Taka ya Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa ziara za viongozi katika maeneo ya miradi zinawapa nguvu ya kufanya kazi zaidi. Amesema kupitia ziara hizo changamoto zinazojitokeza katika miradi zinapata majibu.

Ziara ya Naibu Waziri wa Maji katika mradi wa maji wa Chalinze imelengakuona maendeleo ya ujenziwa mradi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama, na yenye uhakika. Mradi wa Maji wa Chalinze unatarajiwa kutoa huduma kwa wananchi zaidi yaelfu 30.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano

24 Januari, 2019