Habari

Imewekwa: Dec, 14 2018

Naibu Waziri Aweso Avunja Kamati ya Maji Rutemba

News Images

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amevunja kamati ya maji katika Mradi wa Maji Rutemba kutokana na utendaji usioridhisha na kusababisha maendeleo ya mradi kusuasua.

Aweso amechukua hatua hiyo mara baada ya kutoridhishwa na uendeshaji wa mradi wa Rutemba, hali inayosababisha wananchi kupata huduma ya maji isiyoridhisha.

Hivyo, kumlazimu kuchukua hatua ya kuivunja kamati hiyo na kuagiza iundwe kamati mpya yenye wajumbe wenye uwezo, uadilifu na uzalendo katika kusimamia mradi huo.

Pamoja na kutembelea mradi huo, pia ametembelea Miradi ya Maji Likwaya na Namangale katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini na kutatua kero za maji kwa wananchi.

Aidha, Naibu Waziri Aweso ametembelea miradi ya Nangumbu na Michenga iliyopo Wilayani Ruangwa na kutoa maagizo kasoro zote za miradi hiyo zirekebishwe na itoe huduma bora kwa wananchi.