Habari

Imewekwa: Jan, 17 2019

MFANYAKAZI BORA WA WIZARA KWA MWAKA 2017 – 2018

News Images

TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Maji imempa tuzo na fedha shilingi milioni 2 mfanyakazi wake bora kwa mwaka 2017 – 2018 ambaye ni Bw. Heriel Msangi kwa kusimamia Maadili ya Utumishi wa Umma na kulinda rasilimali za serikali kuhujumiwa na baadhi ya watu.

Bw. Msangi alisimamia na kuokoa mali za Wizara ambazo zilikuwa zipotee wakati wa ujenzi wa ofisi za Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini —Tunduru na Ofisi ya Jumuiya ya Watumia Maji Likonde — Namtumbo. Pia,uadilifu wake ulisaidia Wizara kushinda katika shauri la madai dhidi ya Mkandarasi M/S Saro Builders Co. Ltd. Ushindi huo umethibitisha kuwepo kwa usimamizi wa rasilimali za Serikali uliotukuka.

Wakati wa ghafla hiyo, Profesa Mkumbo amewaagiza wataalamu wa Wizara ya Maji kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli ya kuzipitia upya sheria na kanuni za utunzaji wa vyanzo vya maji. Katibu Mkuu amewaelekeza wataalamu wa wizara watafute njia nzuri ambazo rasilimali za maji zitakua endelevu na rafiki kwa jamii inayozizunguka. Amesisitiza rasilimali zisiumize wananchi na wananchi wasiumize rasilimali.

Wizara ya Maji kupitia bodi za mabonde ya maji ina jukumu la kuhakiki na kufuatilia ubora na usalama wa maji katika vyanzo vya maji, kutoa vibali vya kumwaga maji taka, kufuatilia mwenendo wa maji kwenye mito ili maji yawe endelevu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano

17 Januari, 2019