Habari

Imewekwa: Dec, 20 2018

Menejimenti ya Wizara Yatembelea Kuona Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi Katika Mji wa Serikali, Ihumwa Dodoma

News Images

Timu ya Menejimenti kutoka Wizara ya Maji imetembelea eneo la ujenzi wa ofisi ya wizara katika mji wa serikali Ihumwa, jijini Dodoma ambapo maandalizi ya kuweka zege la msingi yamekamilika.

Ujumbe uhuo umeongozwa na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utawala Bw. Stephen Pancras,

Wajumbe wa menejimenti wametembelea eneo hilo ili kuona maendeleo ya ujenzi kama ilivyokubaliwa katika mkataba wa ujenzi.


Ujenzi unatekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT, ambapo msimamizi wa kazi hiyo Mhandisi Juma Ibrahimu amesema ujenzi wa ofisi hizo ulianza rasmi Disemba 7, 2018 na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha siku 60 na hivi sasa maandalizi ya kuweka zege la msingi yamekamilika.

Mtaalam elekezi wa ujenzi huo ni Wakala ya Majengo Tanzania (TBA) kwa ushirikiano na wataalam kutoka Wizara ya Maji wakiongozwa na Mhandisi Tamim Katakweba.

Aidha, timu hiyo ilitembelea ujenzi wa tenki la maji linalojengwa kwa usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA). Tenki hilo lipo katika hatua za mwisho za ujenzi na linauwezo wa kupokea maji lita za ujazo milioni moja.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano

Disemba 20, 2018