Habari

Imewekwa: May, 14 2018

KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI YAKAGUA MIRADI YA MAJI KIGOMA

News Images

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imefanya ziara ya kutembelea mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kukagua miradi ya maji na umwagiliaji inayotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa lengo la kujionea maendeleo na changamoto ya kazi zinazofanywa na wizara hiyo kuelekea Bunge la Bajeti Mwaka 2018/19.

Kamati hiyo imetembelea Manispaa ya Kigoma na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na kujionea mradi mkubwa wa majisafi na majitaka na eneo linalotarajiwa kujengwa skimu ya umwagiliaji.

Ziara hiyo imehusisha wajumbe wa kamati 18 ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mahmoud Mgimwa, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo.