Habari

Imewekwa: Mar, 09 2019

Hali ya Huduma ya Maji Kibondo Mjini

News Images

Wizara ya Maji inafutilia kwa karibu malalamiko kuhusu uchafuzi wa maji Kibondo mjini kama ilivyoripotiwa na baadhi ya wateja katika mabandiko ya mitandao ya kijamii. Ukaguzi wa mfumo wa maji umeanza kwa kuwashirikisha viongozi na wataalam wa maji ambapo huduma ya maji ipo sawa kwa eneo kubwa.

Ukaguzi unawahusisha wataalam kutoka Ofisi ya Idara ya Maji kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji na Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya (CCM).

Wakati ukaguzi unaendelea imeonekana Kanda ya Kumweruro iliyoripotiwa kupata maji machafu bado inasubiri kukamilishwa kwa kisima cha IOM kupitia mradi mpya wa maji wa Kibondo ili kupata huduma ya maji. Aidha, juhudi zinafanyika kurejesha huduma ya maji katika kanda hii baada ya hitilafu ya mfumo wa kusukuma maji.

Aidha, eneo la Kumwai limepata athari kiasi ya mvujo kwa baadhi ya wateja. Wataalam wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kibondo Mjini (KIUWASSA) wanafanyia kazi mvujo huo na ili kurejesha huduma kwa wateja.

Wananchi wa Kibondo mjini wamehakikishiwa huduma bora ya maji na kutakiwa kuwasiliana na KIUWASSA endapo wanataka kutoa mrejesho wakati zoezi la ukaguzi likiendelea.

Imetolwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

09.03.2019