PROF. MAKAME MBARAWA ATEUA WAJUMBE WA BODI YA DAWASA

Imewekwa: Jul 13, 2018


TAARIFA KWA UMMA

Kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria ya DAWASA Na. 20 ya Mwaka 2001, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mheshimiwa Prof. Makame Mnyaa Mbarawa amewateua wajurnbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es Salaam (DAWASA).

Uteuzi huu unakamilisha uundwaji wa Bodi ya DAWASA kufuatia Rais wa Jarnhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kurnteua Jenerali (Mst.), Davis Mwamunyange kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo kuanzia tarehe 7 Julai, 2018.

Kufuatia uteuzi huu, sura kamili ya Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA ni kama ifuatavyo:

1. Jenerali (Mst.) Davis Mwamunyange Mwenyekiti

2. Mhandisi Nadhifa Kemikimba Mjumbe

3. Bwana Edward Paul Mhede Mjumbe

4. Bi. Spora Jonathan Liana Mjumbe

5. Bwana Zuberi Mhina Samataba Mjumbe

6. Dkt. Fred Ben Msemwa Mjumbe

7. Mhandisi Gaudence M. Aksante Mjumbe

8. Bi. Rosemary Kasongo Mjumbe

9. Bwana Latson Msongole Mjumbe


Prof. Kitila Mkurnbo

Katibu Mkuu

12 Julai, 2018.