Wasifu

Athumani Shariff

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Athumani Shariff

Bw. Athumani H. Shariff alizaliwa tarehe 11 Februari, 1984 wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani. Ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mt. Augustine Tanzania na Shahada ya Mawasiliano kwa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro.

Pia, amewahi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za taaluma zikiwemo Shule za Sekondari za Anoor, Maawal na Jumuiya na vyuo ambavyo ni Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro, Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam na Chuo cha Uandishi wa Habari na TEHAMA cha Genesis.

Amehitimu Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Kwakifua, wilayani Muheza (1999) na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Usagara, zote mkoani Tanga (2003); Elimu ya Juu ya Sekondari katika Shule ya Ununio, jijini Dar es Salaam (2006).

Bw. Shariff ni mtaalamu wa masuala ya mawasiliano, aliyejitoa kutumia taaluma na weledi wake katika kufanikisha azma ya maendeleo ya taasisi na taifa lake kwa ujumla.