Wasifu

Joash Nyitambe

Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA

Joash Nyitambe

Joash Ezekiel Nyitambe amekuwa Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Wizara ya Majina Umwagiliaji tangu Januari 2008 hadi sasa. Alikuwa Katibu wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji kati ya Novemba 2006 na Desemba 2007. Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Maji, alikuwa Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kati ya Aprili 2000 na Oktoba 2006; Mratibu wa Mfumo wa Kielektroniki wa Menejimenti ya Taarifa na Takwimu katika Tume ya Jiji la Dar es Salaam chini ya Programu Endelevu ya Miji kati ya Mwaka 1998 na Machi 2000. Kabla ya kuhamishiwa kwenye majukumu ya TEHAMA, alikuwa akifanya kazi za Upimaji Ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kati ya Agosti 1994 na Novemba 1996.

Pamoja na kazi za TEHAMA, Bw. Nyitambe pia, amefanya kazi mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuratibu Programu ya Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi katika Sekta ya Maji kama Mjumbe kwenye Kamati ya Taifa ya Uratibu wa Programu hiyo; Mratibu wa Mfumo wa Kielektroniki wa Masuala ya Mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia Programu Endelevu ya Miji; na Mratibu wa Mpango wa Uboreshaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia Mpango wa Uboreshaji wa Serikali za Mitaa. Kuanzia Mwaka 1998 hadi leo, ni Mtaalamu wa TEHAMA kwa ujumla wake akiwa amefanya kazi mbalimbali za TEHAMA kwenye Taasisi za Serikali kama Mshauri au Msimamizi, pamoja na kushiriki katika mafunzo, kongamano,na semina mbalimbali Ndani na Nje ya Nchi tangu mwaka 1994 kama Mwezeshaji au Mshiriki.

Bw. Nyitambe ana Shahada ya Uzamili katika TEHAMA na Uongozi kutoka Chuo Kikuu cha Avinashilingam, nchini India, ikiwa ni programu ya pamoja na Chuo cha Fedha, Dar es Salaam, nchini Tanzania (Nov, 2006); na Shahada ya Uzamili katika Utengenezaji wa Mifumo ya Kielektroni ya Taarifa za Kijiografia kutoka Chuo cha ITC, nchini Uholanzi (Dec, 1997). Pia ana Stashahada ya Juu ya TEHAMA kutoka Chuo cha City & Guilds, kilichopo nchini Uingezeza (2004), na Stashahada ya Juu ya Upimaji Ardhi kutoka Chuo cha Ardhi, Dar es Salaam (1993). Alizaliwa tarehe 25/12/1966 nabaadaye kujiunga na Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Charya iliyopo katika Wilaya ya Rorya kuanzia mwaka 1975 hadi 1981; elimu ya Sekondari Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Nyakato, mkoani Kagera mwaka 1982 hadi 1985; Elimu ya Juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Mazengo mkoani Dodoma mwaka 1986 hadi 1988. Aidha, kati ya mwaka 1988 na 1989 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mujibu wa Sheria (Operesheni Miaka 25 ya JKT) katika Kambi ya JKT Bulombora, mkoani Kigoma na kumalizia mafunzo hayo katika Kambi ya JKT Buhemba, mkoani Mara.