Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Waziri Lwenge akutana na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini

Swahili

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge amekutana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini (Charge d’Affaires), Inmi Patterson ofisini kwake kuzungumza namna ya kusaidia kuinua Sekta za Maji na Umwagiliaji Nchini. Katika mazungumzo hayo Waziri Lwenge alisema bado kuna nafasi kubwa ya uwekezaji kwenye maeneo ya kusambaza huduma ya majisafi na majitaka, ujenzi wa mabwawa na mifumo ya kuvuna maji ya mvua, pamoja na kilimo cha umwagiliaji na kuiomba Serikali ya Marekani kutoa kipaumbele katika maeneo hayo.

“Tunaishukuru Serikali ya Marekani ambayo imeendelea kuwa msaada mkubwa kwenye Sekta yetu ya Maji nchini, kupitia utekelezaji wake wa miradi ya maendeleo yenye tija kubwa; hususani katika kuondoa kero ya huduma ya majisafi, lakini pia bado kuna fursa nyingi za uwekezaji kama kwenye kilimo cha umwagiliaji, huduma ya majitaka na ujenzi wa mabwawa ya kuhifadhi maji”, alisema Inj. Lwenge.

“Tuko tayari kushirikiana na Marekani ili kuleta maendeleo katika maeneo hayo, ambayo yatakuwa ni chachu kubwa maendelo ya uchumi wa taifa letu na kwa wananchi wote wa mijini na vijini”, alisisitiza Waziri Lwenge. Wakati huo, Kaimu Balozi wa Marekani, Inmi Patterson alitoa pongezi kwa Serikali ya Tanzania inavyosimamia vyema fedha za misaada inazopokea kutoka kwa wafadhili na kuwa waaminifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambayo inayoonekana. Na kuahidi wako tayari kusaidia maeneo yalioanishwa na Waziri Lwenge na kuleta maendeleo ya sekta hizo muhimu nchini.

Photo: