Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Waziri Kamwelwe Azindua Miradi ya Shilingi Bilioni 2.76 Mtwara

Swahili

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua miradi miwili ya maji ambayo ipo Halmashauri za Wilaya ya Mtwara na Masasi Mkoani Mtwara ilyogharimu jumla ya shilingi bilioni 2,764,376,293.19 yote kwa pamoja.  Mradi wa maji wa Mayaya katika Halmashauri ya Mtwara uligharimu shilingi 973,022,925 una vituo 37 vya kuchotea maji na unanufaisha wananchi wapatao 4,997. 

 Katika Halmashauri ya Masasi Waziri Kamwelwe alizindua mradi wa maji wa Shaurimoyo– Mpindimbi wenye thamani ya shilingi 1,791,353,368.19 ambao utanufaisha wakazi wapatao 8,400 washio katika vijiji vya Shaurimoyo, Kachepa, Mpindimbi na Kanyimbi.  Wakati wa uzinduzi wa Miradi hiyo, wananchi walishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo kwani walikuwa na adha kubwa ya maji ambapo kabla ya mradi walikuwa wakinunua ndoo moja ya lita 20 kwa shilingi elfu moja na baada ya mradi wananunua ndoo moja kwa shilingi hamsini tu.

 Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Lulindi Jerome Bwanausi amemshukuru Waziri wa Maji na Umwagiliaji na serikali ya awamu ya tano kwa kukamilisha ahadi zao, na ana furaha isiyo na kifani kwa kukamilika miradi hiyo ambayo imeondoa kero kubwa ya maji kwa wananchi.

Photo: