Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Utaratibu wa Kufanyiwa kazi ya Uchunguzi wa Ubora wa Maji kwenye Maabara za Maji

Tuesday, December 30, 2014 - 11

Utaratibu wa Kufanyiwa kazi ya Uchunguzi wa Ubora wa Maji kwenye Maabara za Maji zilizo Chini ya Wizara ya Maji- Idara ya Huduma za Ubora wa Maji 

Uchunguzi wa usafi na ubora wa maji ni huduma muhimu inayofanywa na wataalamu wa ubora wa maji kwa kutumiavifaavya kisayansi vya kupimia ubora wa maji kwa matumizi mbalimbali,  na pia kubaini mwenendo wa ubora katika vyanzo nakwenye mfumowa usambazaji wa maji ya kunywa. Maji kutoka chanzo chochote kipya ni lazima yafanyiwe uchunguzi kabla ya kuanza kutumika; pia ubora wake uendelee kufuatiliwa kulingana na utaratibu uliowekwa katika kuhakiki ubora wa maji hayo. Taarifa ya uchunguzi wa ubora wa maji ni ya muhimu kwa mteja kwa ajili ya kujihakikishia usafi na usalama wa maji ya chanzo chake katika kulinda afya za watumiaji wa maji kutoka kwenye chanzo husika.

Kwa maelezo zaidi bofya hapa