Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

TAARIFA KWA UMMA

Mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa Victoria Awamu ya Pili kwa kushirikiana na Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ambayo ni taasisi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, imeandaa Kongamano la Utafiti wa Kisayansi la Bonde la Ziwa Victoria litakalofanyika kuanzia tarehe 15 – 16 Februari, 2017 katika Hoteli ya Malaika Beach Resort, jijini Mwanza, Tanzania. Kauli mbiu ya Kongamano ni “Matumizi ya Tafiti na Sayansi katika kuimarisha Usimamizi wa Rasilimali za Maji Shirikishi katika Bonde la Ziwa Victoria”.

Kongamano litawakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo watafiti kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi nyingine, ili kubadilishana uzoefu katika maeneo ya Usimamizi endelevu wa Rasilimali za Maji na Uvuvi; Masuala ya Kijamii; Kiuchumi na Kisera; Udhibiti wa uchafuzi wa Mazingira na Maendeleo Endelevu ya Kilimo katika Bonde la Ziwa Victoria na mabadiliko ya Tabia Nchi.

Aidha, mada za tafiti mbalimbali kuhusu Bonde la Ziwa Victoria zitawasilishwa, ambapo washiriki watapata fursa ya kuchangia, pamoja na kutoa mapendekezo ya uhifadhi na matumizi endelevu ya Rasilimali za Bonde la Ziwa Victoria. Pia, kutakuwa na maonesho ya shughuli mbalimbali za uhifadhi wa mazingira na kukuza uchumi.  

Wadau wote kutoka Taasisi za Kiserikali, Mashirika ya Umma, Wabia wa Maendeleo, Asasi za Kiraia, Taasisi zisizo za Kiserikali, Sekta Binafsi, Vyuo Vikuu, Watafiti na wadau wote mnakaribishwa kushiriki katika kongamano hili. Washiriki wanatakiwa kujiandikisha na kulipia ada ya ushiriki Dola za Kimarekani 104 kupitia tovuti https://www.lvbcom.org/register/ au siku moja kabla ya kongamano katika Hoteli ya Malaika Beach Resort. Kwa wadau watakaohitaji kufanya maonesho watatakiwa kulipia Dola za Kimarekani 200 katika Akaunti ya LVEMP II-9120000371929, Benki ya Stanbic Tawi la Mwanza.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu Na. +255784813841 au tuma baruapepe kwa mwanamkuu.zmwanyika@maji.go.tz na lilian.batao@maji.go.tz.