Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Naibu katibu Mkuu aungana na wanakijiji kuchimba mitaro ya kulaza bomba la maji

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Eng. Emmanuel Kalobelo aliungana na wanavijiji vya Chiyapi, Litama, Naipanga, Mailisita na Mkotokuyana kuchimba mitaro itakayotumika kulaza bomba la maji kutoka mradi wa maji wa Masi- Nachingwea.

Katika ziara hayo Naibu Katibu Mkuu sambamba na kushiriki katika zoezi la uchimbaji mitaro, aliwahamasisha wananchi hao juu kuongeza kasi ya uchimbaji mitaro ili kazi ya ulazaji wa mabomba ianze mara moja. Pia aliwashukuru kwa namna wanalivyoamua kujitolea kufanya kazi hiyo bila malipo. Aidha aliwataka kuhakikisha wanalinda miundombinu ya maji kwa kuwa serikali imeona umuhimu wa maji na kutenga fedha kwa ajili ya miradi hiyo ambapo ingeweza kupeleka fedha hizo katika sekta nyingine muhimu.

Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Wizara ilitenga kiasi cha shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya kufikisha maji katika vijiji vilivyo kando kando ya bomba kuu la mradi wa maji Masasi - Nachingwea. Katika mpango huo, vijiji vilivyopewa kipaumbele ni Chiyapi, Nandanga, Ipingo, Lucheregwa na Litama vilivyo katika Wilaya ya Ruangwa, Vijiji vya Mtepeche, Magereza, Mailisita, Mkotokuyana na Naipanga vilivyo katika Wilaya ya Nachingwea na Vijiji vya Maparagwe, Namakongwa, Chikukwe, Mbemba, Mkuyuni na Mbaju vilivyo katika Wilaya ya Masasi.Utekelezaji wa mradi huu umeanza tarehe 30 Julai, 2017 ambapo kwa sasa wakazi wa vijiji husika wapo katika hatua ya uchimbaji mitaro itakayotumika kulaza mabomba. Vijiji ambavyo vimekamilisha uchimbaji wa mitaro ni kijiji cha Naipanga, Mailisita na Mkotokuyana ambavyo vipo katika Wilaya ya Nachingwea. Vijiji vya Chiyapi, Litama, Luchelegwa, Nandanga na Ipingo vinaendelea na kazi ya uchimbaji mitaro. Kazi ya ulazaji wa mabomba itaanza mara baada ya kazi ya uchimbaji mitaro kukamilika. Tayari bomba za kipenyo cha nchi mbili zenye urefu wa mita 7,500 na bomba za kipenyo cha inchi tatu zenye urefu wa mita 3,912 sawa na vipande 65 zimewasili