Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mwongozo wa Matumizi salama yaVifaa na Mifumo ya TEHAMA

Mwongozo huu umeandaliwa kwa kuzingatia mazingira ya Wizara ya Maji katika kulinda usalama wa taarifa na kumbukumbu za Serikali ikiwa ni utekelezaji wa Waraka wa Utumishi Na. 5 wa Mwaka 2009 na Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi, na Salama ya Vifaa na Mifumo Menejimenti ya Utumishi wa Umma Julai 2012. Mwongozo unatokana na ukweli kwamba kuna ongezeko kubwa la matumizi ya TEHAMA katika kuboresha utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi. Vilevile, mwongozo huu unalenga kuweka utaratibu mzuri na wenye tija katika kuanzisha, kutekeleza na kutumia vifaa na Mifumo ya TEHAMA ili kuwa na ufanisi katika kutekeleza Awamu ya Pili ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji iliyozinduliwa na Mheshimiwa Waziri wa Maji tarehe 22 Septemba 2014. Mwongozo huu unahimiza watumishi wa Wizara ya Maji katika ngazi zote kufuata maelekezo na utaratibu bora katika matumizi ya TEHAMA ikiwemo matumizi ya barua pepe, vitunza kumbukumbu, mifumo ya kielektroniki na huduma za mtandao.

Kwa maelezo zaidi bofya hapa