Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mradi wa Wanging'ombe

Mradi huu unaoendeshwa kwa nguvu za mtiririko wa asili. Ulijengwa miaka ya 1980 ulifadhiliwa na UNICEF iliyochangia kiasi cha dola za Kimarekani 5,486,000, na Serikali ya Tanzania iliyochangia kiasi cha Sh.15,000,000/=

Mradi huu uko katika Wilaya ya Njombe katika Mkoa wa Iringa ukiwa na eneo la Kilomita za mraba 1000. Mradi una matoleo mawili ya maji ya Mbukwa na Mtilafu yenye uwezo wa lita milion 6.70 na 6.0. Mpaka sasa mradi unahudumia vijiji 60 vituo 574 vya jamii na vifuo 568 zimeunganishwa. Mradi una matanki 54 ya kuhifadhi maji yenye ujazo wa kati ya 50m3 na 150m3.