Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mradi wa Mgango/Kiabakari

Mradi wa Maji wa Mgango/Kiabakari/Butiama unasimamiwa na Bodi iliyoanzishwa tarehe 30/01/2004 na wajumbe wa Bodi waliteuliwa na Waziri wa Maji tarehe 15/05/2004. Mamlaka ilikabidhiwa rasmi kazi ya kuendesha mradi huu kutoka kwa Mhandisi wa Maji wa Mkoa tarehe 01/09/2004.

Uwezo wa mradi huu ni kuwapatia maji watu wapatao 64,255 katika vijiji 13, kwa sasa ni watu 38,553 tu wanaopata maji kwa umbali usiozidi mita za ujazo 400 ambao ni asilimia 60 tu ya watu waliotarajiwa. Maji yanayosambazwa ni mita za ujazo 4,157 kwa siku wakati mahitaji halisi ni m3 5,576 kwa siku.