Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mradi wa Makonde

Mradi huu unahudumia maeneo ya Newala, Tandahimba na vijiji 14 vya Kata ya Nanyamba Wilaya Mtwara vijijini katika Mkoa wa Mtwara.

Mradi huo una hudumia wananchi wa Wilaya za Mtwara kwa upande wa Mashariki, Lindi kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Masasi kwa upande wa Magharibi na upande wa Kusini mwa Mto Ruvuma mpakani na Msumbiji. Eneo la Mradi ni zaidi ya 4020km za mraba na idadi ya watu wanaohudumiwa na mradi huo ni zaidi ya watu 408,578.

Makadirio ya uwezo mradi ni kutoa mita za ujazo 23,840 kwa siku na kuhudumia idadi ya watu wapato 347,140.