Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mradi wa Kahama Shinyanga

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia fedha za ndani kupitia Wizara ya Maji imetekeleza mradi wa kutoa maji toka Ziwa Victoria kwa ajili ya matumizi ya wananchi katika miji ya Kahama na Shinyanga na vijiji 58 vilivyo njiani na bomba kuu na migodi ya madini. Mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 242. Mradi huu unalenga kuwapatia majisafi na salama ya kutosha kwa sasa watu wapatao 450,000 kwa kusambaza kiasi cha mita za ujazo 80,000 kwa siku. Mradi unategemewa kuongeza usambazaji wa maji hadi kufikia mita za ujazo 120,000 kwa siku na kuwapatia maji watu wapatao milioni moja ifikapo mwaka 2025.