Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mradi wa Handeni

Mradi wa Maji wa Handeni uko katika Wilaya Korogwe, na Korogwe katika Mkoa wa Tanga, ukiwa na eneo la kilometa za mraba 5000. Kilometa 316 ni truck main, kilometa 100 ni matawi ya mradi, vituo vya pampu sita, matanki ya kuhifadhi maji 56, vituo vya kuchotea maji 163, na waliunganisha mitandao ya maji 703. Mradi unahudumia vijiji 79 ukiwemo mji wa Handeni wenye idadi ya watu 180.

Mradi huu una matoleo mawili kutoka Mto Pangani na kuyasukuma kwa kutumia nguvu za mtiririko asilia au nguvu za mashine. Toleo la Mandela (Tabora) linapeleka maji katika mtambo wa kusafisha maji wa “Slow Sand Filltes” unaochukua kiasi cha 2300 m3 kwa siku na toleo la Mkumburu (Segera) linachukua kiasi cha 170m3 kwa saa (4,080m3 kwa siku).