Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mradi wa Chalinze

Utekelezaji wa mradi wa Chalinze ulianza mwaka 2001 ukiwa na lengo la kuwapatia watu 105,000 maji safi na salama ifikapo mwaka 2015. Ujenzi wa mradi huo ulikamilika mwaka 2003, lengo ni kuvipatia huduma ya maji vijijini 20. Mradi huo ulifadhiliwa na Serikali ya China kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Awamu ya kwanza ilikuwa kwa ajili ya vijiji 18 baada ya kukamilika kwa mradi. Vijiji vilivyokuwa katika awamu ya kwanza ni Chalinze, Pingo, Msoga, Mboga, Lugoba, Saleni, Mazizi, Msata na Kihangaike kwa upande wa Kusini. Upande wa Kaskazini, vijiji vilivyokuwemo ni Mandera, Hondogo, Kilemela, Miono, Kikaro, Rupungwi, Kimage na Mbwewe. Utekelezaji wa mradi huo uko katika awamu ya pili unaendelea.