Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi

Mpango wa Uendeshaji Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP) ni juhudi ya Kimataifa inayolenga kuhimiza uwazi, kuwawezesha wananchi, kupambana dhidi ya rushwa na kuhimiza kutumia teknolojia mpya na kuboresha utawala. OGP ilizinduliwa rasmi tarehe 20 Septemba 2011 mjini New York na nchi 8 wanachama waanzilishi za Brazili, Indonesia, Mexico, Norway, Philippines, Afrika Kusini, Uingereza na Marekani. OGP inasimamaiwa na Kamati ya Uendeshaji ya Kimataifa ya wadau mbalimbali yenye wawakilishi wa Serikali na Asasi za kiraia.

Tembelea Tovuti ya  OGP ili kufahamu  Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi

http://www.opengov.go.tz/