Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Majukumu makuu ya Wizara ya Maji yamegawanywa kwa kuzingatia Muundo wa Wizara kama ifuatavyo:-

 

  • Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa Sera, Mikakati na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji.
  • Kutayarisha na kusimamia sheria, kanuni na taaratibu zinazosimamia Sekta ya Maji;
  • Kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji;
  • Kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kuhifadhi takwimu muhimu za Sekta ya Maji;
  • Kutoa miongozo ya kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za maji;
  • Kutoa miongozo ya utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira vijijini na mijini;
  • Kutoa mafunzo kwa Wataalam wa Sekta ya Maji katika ngazi na kada mbalimbali za utekelezaji;
  • Kuendeleza tafiti kuhusu teknolojia bora zinazotumika katika kutoa huduma ya maji;
  • Kuratibu majukumu na kutekeleza ushauri wa Bodi ya Taifa ya Maji