Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Maandalizi ya Utunzaji wa Vyanzo vya Maji Mito ya Ruvu na Zigi Yaiva

Thursday, October 23, 2014 - 15

Kaimu katibu mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba leo amefungua warsha ya siku moja itakayojadili taarifa ya maandalizi ya rasimu ya andiko la mradi wa utunzaji vyanzo vya mito ya Zigi Mkoani Tanga na Ruvu Morogoro. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam ina lengo la kujadili kwa undani changamoto na fursa mbambalimbali katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji za vidakio maji vya mito ya Ruvu and Zigi kwa kushirikisha sekta zinazohusiana na maji pamoja na taasisi binafsi na zisikuwa za kiserikali.

Idara ya Rasilimali za Maji Wizara ya Maji kwa kushirikiana na UNDP ilipata fedha kutoka Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF) jumla ya Dola za Kimarekani (US$) 300,000 sawa na Tshs. 480,000,000.00 kwa ajili ya maandalizi ya Mradi (Project Preparation Grant) wa utunzaji wa vyanzo vya maji. Idara ya Rasilimali za maji kwa sasa ipo katika mchakato wa kuandaa andiko la Mradi wa utunzaji wa vidakio maji kwa kuanzia (pilot) vidakio vya Mito ya Ruvu na Zigi; ‘‘Securing Watershed Services through Sustainable Land Management in the Ruvu and Zigi Catchments (Eastern Arc Region)’’. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba amesema, ni lazima kushirikiana katika utunzaji wa vyanzo vya maji. “Kitu ambacho ni lazima nikiseme kwenu, imekuwa vizuri warsha hii kukusanyisha wadau wote muhimu, kwani utunzaji wa vyanzo vya maji ni kazi za wadau wote” alisema Futakamba.

Inj. Futakamba aliwataka washiriki wa warsha hiyo watumie muda huo vizuri ili kujadili kwa kina ili matumizi ya maji na ardhi yafanyike kwa weledi zaidi kwa mafanikio ya maisha ya watu. Matokeo ya Warsha hiyo ni kupata maoni ambayo yatasaidia kumalizia Andiko la Mradi tayari kwa utekelezaji wa mradi huo ambao umepangwa ketekelezwa kuanzia mwaka 2014 hadi 2020. Warsha hiyo itahusisha Washiriki 80 kutoka Wizara ya Maji, Maofisa kutoka Sekretariati za Mikoa ya Morogoro na Tanga, Maofisa kutoka Halmashauri za Wilaya za Morogoro Vijijini, Mvomero, Muheza, Tanga, Mkinga, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maofisa wa Maji wa Mabonde (Bonde la Pangani na Wami/Ruvu), Tume ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi, Taasisi zisizo za kiserikali (IWASH,EAMCEF, MVIWATA, SAT, Uluguru Nature Reserve, Amani Nature Reserve, n.k.), Wawakilishi kutoka DAWASA, DAWASCO, Tanga UWASA, TAFORI pamoja na Wawakilishi kutoka vyama vya watumia maji UWAMAKIZI, UWAMFIZIGO