Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Maji ya Afrika na Mkutano Mkuu wa Kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika Utakayofanyika Nchini Tanzania

Baraza la Mawaziri wa Maji Afrika (AMCOW) linalofanya kazi pamoja na Tume ya Umoja wa Afrika chini ya Idara ya Uchumi Vijijini na Kilimo (AUC-DREA) na Nchi Wanachama wanafanya harakati za kuhakikisha lengo la Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira linafikiwa ulimwenguni. Azma hii imelenga kuhakikisha kunakuwa na misingi imara ya usimamizi, utunzaji na uendelezaji wa rasilimali za maji kwa ajili ya wote, pamoja na hatua sahihi za usafi wa mazingira na afya ya mwanadamu. 

Sekretarieti ya AMCOW kwa kushirikiana na Wizara ya Maji na Umwagiliaji itaandaa Maadhimisho ya 6 wa Wiki ya Maji ya Afrika na Mkutano Mkuu wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika, jijini Dar es Salaam, Tanzania chini ya kaulimbiu isemayo 'Kufikia Lengo la Maendeleo Endelevu (SDGs) juu ya Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira'.

Kwa maelezo zaidi bonyeza hapa