Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kitengo cha Uratibu wa Programu

Utangulizi

Uratibu wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji unasimamiwa na Wizara ya Maji kupitia Kitengo kilichoanzishwa mahsusi kwa ajili ya uratibu wa Programu. Kitengo hicho kinawajibika moja kwa moja kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kuanzia 
mwezi Oktoba, 2010. Kuanzia mwezi Septemba, 2011 Mkuu wa Kitengo amepewa hadhi ya Mkurugenzi kulingana na muundo huo. Naibu Katibu Mkuu atatoa miongozo husika kwa Kitengo na:-

(i) Kusimamia utekelezaji wa Programu kulingana na makubaliano ya Mkataba wa Ushirikiano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo;
(ii) Kuratibu majadiliano na wadau katika sekta ya maji, wakiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Wizara ya Fedha, na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii; na 
(iii) Kuhakikisha utendaji wenye tija kati ya wadau muhimu, ikiwemo Wizara ya Maji, Watekelezaji wa Miradi na Washirika wa Maendeleo.

Jukumu kubwa la Kitengo cha Uratibu wa Programu ni kuhakikisha malengo ya Programu yanatekelezwa kwa ufanisi mkubwa, na kuzingatia value for money.

Kazi za Kitengo cha Uratibu ni pamoja na:-

(i) Kuratibu upatikanaji na usambazaji taarifa zote zinazohusiana na Programu;
(ii) Kuandaa na kutumia miongozo ya kiufundi kwa ajili ya utekelezaji wa Programu;
(iii) Kuhakikisha Programu inatekelezwa kama ilivyokubalika katika Mkataba kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo;
(iv) Kushauri kuhusu utekelezaji na utendaji wa wadau muhimu ikiwemo, Serikali, Washirika wa Maendeleo na vyombo vingine vya maamuzi;
(v) Kudurusu Programu ya Maendeleo ya Maji ili iendane na Sera nyingine za nchi, hususan MKUKUTA II; na 
(vi) Kuratibu ushirikiano kati ya Programu hii na nyingine, zikiwemo za Sekta ya Kilimo, Maboresho ya Sekta ya Afya na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu.