Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kinaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani

kazi zake ni:

 Kuandaa mpango mkakati wa ukaguzi.
 Kuratibu kazi za ukaguzi.
 Kutoa ushauri kwa Afisa Msuuli katika matumizi ya fedha.
 Kufanya ukaguzi wa vifungu vya fedha na wale wote wanaopokea fedha ya Wizara.
 Kuweka sawa mifumo ya uhasibu, uhakiki wa malipo na ukusanyaji wa risiti.
 Kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
 Kupitia taarifa za ukaguzi wa ndani na nje kwa kushirikiana na uongozi wa juu Wizarani.