Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kitengo cha Teknohama

Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kinaongozwa na Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta.

Kazi za Kitengo:

 Kusimamia utekelezaji wa sera ya Serikali Mtandao na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Wizara.
 Kuhakikisha vifaa vya kompyuta na mtandao wa mawasiliano vinakuwa katika hali nzuri.
 Kusaidia na kutoa huduma za manunuzi ya vifaa vya kompyuta na Mtandao wa Mawasiliano katika Wizara.
 Kuanzisha na kusimamia matumizi ya mawasiliano ya baruapepe, mtandao wa ndani na nje ya Wizara.
 Kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa mifumo ya kompyuta na benki za takwimu katika Wizara.
 Kuratibu na kusimamia uendelezaji wa watumishi katika matumizi ya Technolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA).
 Kufanya tafiti zinazohusiana na utumiaji wa teknolojia ya mawasiliano kama chombo cha kuimarisha utendaji, utoaji wa taarifa muhimu na huduma kwa wananchi na wadau wote.