Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kitengo cha mawasiliano serikalini

Kitengo kinaongozwa na Afisa Habari Mkuu

Kitengo kinatoa huduma ya upatikanaji wa taarifa, mawasiliano ya Wizara kwa umma na vyombo vya habari.

Kazi zake:

Kuandaa na kutoa machapisho, vipeperushi, makala, majarida n.k. kwa lengo la kuhamasisha umma juu ya Sera, programu, kazi na mabadiliko yanayotokea ndani ya Wizara.
Kuratibu mazungumzo ya Wizara na vyombo vya habari.
 Kushiriki katika mijadala ya Wizara na umma pamoja na vyombo vya habari.
 Kuhamasisha utekelezaji wa sera na programu za Wizara.
 Kuratibu maandalizi ya taarifa mbalimbali zinazotolewa kwenye makongamano, mikutano, na vyombo vya habari.
 Kuratibu uandaaji na utoaji wa jarida la Wizara.
 Kuratibu uwekaji wa taarifa katika tovuti ya Wizara.