Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kitengo cha Manunuzi

Kitengo cha Manunuzi kinaongozwa na Afisa Ugavi Mkuu.

Kitengo kinajukumu la kutoa huduma na utaalamu katika masuala ya manunuzi, uhifadhi na usambazaji wa huduma na bidhaa kwa Wizara.

Kazi zake:

 Kutoa ushauri kwa menejimenti katika masuala ya manunuzi ya vifaa na huduma.
 Kuhakikisha kuwa Wizara inazikubali taratibu na kanuni za manunuzi kutokana na sheria ya umma ya manunuzi Na.21 ya 2004.
 Kuandaa mpango mwaka wa manunuzi wa Wizara.
Kununua na kusimamia usambazaji, malighafi na utoaji wa huduma ili kusaidia mahitaji ya Wizara.
 Kuhakikisha kuwa uhifadhi mzuri na usambazaji wa vifaa vya ofisi unatekelezwa kwa muda muafaka.
 Kuwa Katibu wa Bodi ya Manunuzi kama Kanuni za umma za manunuzi zinavyosema.
 Kusaidia Idara na vitengo vya Wizara kupata ubora wa vitu kulingana na bei, ubora na ufikishwaji wa huduma na bidhaa zinazohitajika