Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idara ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu

Idara ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu inaongozwa na Mkurugenzi.

Kazi zake ni:
 Kutoa mikakati ya kimenejimenti katika utawala na maendeleo ya rasilimali watu kama vile kuajiri, mafunzo, kuhamasisha kutoa huduma kwa watumishi na usimamizi wa katika utendaji;
 Kuhakiki usimamizi wa rasilimali watu katika Wizara;
 Kuunganisha kati ya Wizara na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika utendaji wa menejimenti ya utumishi wa umma;
 Kutoa huduma ya maelezo na kutunza kumbukumbu za taarifa za rasilimali watu.

Sehemu ya Usimamizi ni:

 Kutafsiri kanuni za huduma za umma, kanuni Standing Order na sheria zingine za kazi;
 Kusimamia uhusiano mzuri wa wafanyakazi na ustawi pamoja na afya, usalama, michezo na utamaduni;
 Kutoa usajili, kuweka kumbukumbu za Ofisi na huduma za wahudumu;
 Inasimamia masuala ya kanuni.
 Kutoa huduma za ulinzi, usafiri na mambo mengine ya kiutawala kwa ujumla;
 Kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo jinsia, wasiojiweza, Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi;
 Kufuatilia utekelezaji wa ushiriki sekta binafsi katika Wizara;
 Kusimamia jukumu la utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa wateja wa Wizara.

Sehemu ya menejimenti ya Rasilimali Watu

 Inasimamia zoezi zima la ajira ikiwemo kukusanya, kuchagua, kuchukua, kuthibitisha kazini pamoja na uhamisho;
 Inahusika na maendeleo na mafunzo ya rasilimali watu;
 Inasimamia mafunzo ya awali na programu za utangulizi kwa waajiriwa wapya;
 Kuweka mipango ya rasilimali watu ili kujua mahitaji na idadi ya wataalamu walio chini ya Wizara;
 Kusimamia mishahara na kuandaa idadi ya watu wote walioajiriwa;
 Kusimamia utekelezaji wa malengo na mfumo wa wazi wa kupima utekelezaji wa watumishi wa Wizara.