Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idara ya Sera na Mipango

Idara ya Sera na Mipango inaongozwa na Mkurugenzi.
Idara ina sehemu tatu:

Majukumu ya Idara hii ni kuandaa Sera kusimamia utekelezaji wake na kupima matokeo ya utekelezaji wa Sera.

Kazi zake ni:
 Kusimamia maandalizi ya bajeti ya Wizara;

Kusimamia na kupima utekelezaji wa shughuli za Sekta ya Maji  ndani na nje ya Wizara ili kuona kama vigezo vya utekelezaji vilivyowekwa vinafuatwa;
 Kutoa miongozo ya kimaamuzi ya mipango ya baadaye ya Wizara;
 Kuhamasisha na kuwezesha sekta binafsi ili ziweze kuwekeza katika sekta ya maji;
 Kukusanya taarifa za sekta za maji  kwa ajili ya maamuzi ya Wizara;
 Kuhusika na maandalizi ya Hotuba ya Wizara na taarifa ya mwaka ya hali ya uchumi;
 Kutoa utaalamu wa mkakati wa pamoja katika kupanga na kubajeti;
 Kuhakikisha mipango na bajeti za sekta za maji zinawekwa katika mipango na bajeti ya taifa.

Sehemu ya Sera:

Kazi zake:

Kuratibu maandalizi na mapitio ya sera za Wizara na kuziwianisha na Sera nyingine za Kitaifa;

Kuratibu utoaji wa maoni na ushauri kuhusu Sera na Nyaraka za Baraza la Mawaziri zilizoandaliwa na Wizara nyingine.

Kuandaa (memorandum of understanding) za miradi na programu kwa ajili ya ushirikiano na utafutaji wa fedha kimataifa;

Kuandaa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na maoni ya Kamati za Bunge; na

Kuratibu maandalizi ya Hotuba ya mwaka ya mpango wa bajeti wa Wizara.

Sehemu ya Mipango

Kazi zake:

Kuratibu uandaaji wa mpango wa mwaka na bajeti ya Wizara kwa utekelezaji na mpango mkakati wa muda wa kati;

Kuunganisha taarifa za miradi ya maendeleo, program na mpango wa utekelezaji;

Kuandaa mikakati ya utafutaji fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo;

Kuwasiliana na Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais –Tume ya Mipango na ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma kuhusu mipango na bajeti ya Wizara na taratibu za upangaji wake;

Kutoa miongozo ya kitaalam na kusaidia ujenzi wa uwezo kwa Wizara kuhusu uandaaji wa mpango mkakati na bajeti; na

Kushiriki katika uchambuzi na uhamasishaji wa kazi zinazoweza kufanywa na sekta binafsi.

Sehemu ya Usimamizi na ufuatiliaji

Kazi zake:

Kufuatilia utekelezaji wa mpango wa mwaka na mpango mkakati wa muda wa kati wa Wizara;

Kuandaa taarifa za utekelezaji (za wiki, mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na za mwaka mzima za Wizara);

Kukusanya, kutafiti na kuchambua takwimu muhimu zinazohitajika katika uandaaji na utekelezaji wa Sera, mipango na bajeti.

Kushiriki katika maandalizi ya mipango,  programu na kazi za Wizara ikiwemo utengenezaji wa malengo na viashiria vyake.

Kutoa msaada wa kiufundi ndani ya Wizara, hii ni pamoja na usimamizi na ufuatiliaji katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara;

Kufanya ufuatiliaji wa huduma inayotolewa na Wizara kwa Wadau;

 Kufanya tafiti na tathmini ya mipango, miradi na program za Wizara; na

 Kufuatilia utendaji wa wakala za Wizara.

Kuratibu mapitio ya utekelezaji wa majukumu yaWizara