Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idara ya Rasilimali za Maji

Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi.

Majukumu yake ni kusimamia na kufuatilia wingi na ubora wa rasilimali za maji pamoja na usalama wa mabwawa. Vilevile Idara hukusanya takwimu za kihaidrolojia na za matumizi ya maji, kuandaa ramani za kihaidrolojia, huandaa vibali vya matumizi ya maji; ukaguzi wa vyanzo vya maji na kuweka mipango ya utafiti wa vyanzo vya maji pamoja na usimamizi wa mazingira ya vyanzo vya maji na kutoa msaada wa kiufundi na elimu ya uhamasishaji juu ya ujenzi wa visima, uhandisi wa masuala ya maji, usimamizi wa maeneo ya matukio na matumizi sahihi ya vyanzo vya maji.

Kazi za Idara

 Kusimamia na kuandaa Sera ya Maji pamoja na utekelezaji wake;
 Kusimamia matumizi endelevu ya maji;
 Kusimamia maendeleo na usimamizi sahihi wa vyanzo vya maji kulingana na sera na mikakati;
 Kukusanya taarifa za kihaidrojeolojia na kihaidrometolojia na kuzisambaza kwenye taasisi za Serikali na umma;
 Kuzijengea uwezo Sekretariati za Maji;
 Kuratibu ushiriki wa Wizara katika mijadala ya kitaifa na kimataifa ya maendeleo, usimamizi pamoja na matumizi ya rasilimali za maji shiriki;
 Kutoa miongozo kwa wadau kuhusu usanifu na ujenzi wa mabwawa na usimamizi wa hifadhi za maji.

Idara ina sehemu tatu na Bodi ya Maji iko chini ya Idara hii:

Sehemu ya Usimamizi na Tathmini ya Rasilimali za Maji

Kazi zake:
 Kutoa miongozo na viwango vya upatikanaji wa takwimu za kihaijeolojia na kihaidrometolojia;
 Kusimamia Benki ya Takwimu za rasilimali za maji za hapa nchini;
 Kusimamia kazi za Ofisi za Mabonde na kutoa msaada wa kiufundi katika kusimamia, kuratibu na kuendeleza kazi za rasilimali za maji;
 Kutoa miongozo na viwango vya usanifu na ujenzi wa mabwawa;
 Kuwasiliana na wakala wa hali ya hewa Tanzania juu ya utabiri wa hali ya hewa pamoja na mifumo ya tahadhari na kuzitawanya taarifa kwa umma.

 

Sehemu ya Mipango Utafiti na Maendeleo ya Rasilimali za Maji
Kazi zake ni:
 Kuratibu mipango shirikishi ya maendeleo na matumizi ya maji katika Sekta ya Maji;
 Kutafiti na kuendeleza vyanzo mbalimbali vya maji;
 Kuhifadhi na kusambaza taarifa mbalimbali za vyanzo vya maji;
 Kuratibu na kufanya tafiti zinazohusiana na ya maendeleo ya vyanzo vya maji.

Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Shiriki
Kazi zake ni:
 Kuratibu ushiriki wa Wizara katika mijadala ya kitaifa na kimataifa inayohusu uanzishwaji wa miradi ya maendeleo na kuendeleza matumizi ya maji shiriki;
 Kuratibu na kuandaa utekelezaji wa miradi na usimamizi wa rasilimali za maji shiriki.

Sehemu ya Uhifadhi wa Vyanzo vya Maji
Kazi zake ni:
 Kutoa miongozo na msaada kwa ofisi za mabonde juu ya utekelezaji wa sheria na matumizi ya maji ikiwemo sheria juu ya uchimbaji visima na utafiti wa maji chini ya ardhi;
 Kusimamia daftari la haki za maji, jumuiya za watumiaji maji na makundi mengineyo na
 Kuratibu na kusimamia shughuli za uhifadhi wa rasilimali za maji.

Bodi ya Maji

Kazi zake ni:
 Kutoa ushauri kwa Waziri juu ya matumizi ya maji kwa watumia maji.