Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idara ya Maji Vijijini

Idara ya Maji kwa Jamii inaongozwa na Mkurugenzi.

Kazi zake ni:
 Kuandaa na kupitia Sera ya Maji pamoja na utekelezaji wa Sera na Mikakati hususan katika masuala ya huduma za maji kwa jamii;
 Kuhamasisha maendeleo ya ukuaji wa huduma ya maji kwa jamii kulingana na Sera na Mkakati;
 Kusimamia utekelezaji wa programu za huduma ya maji kwa jamii;
 Kuzijengea uwezo Sekretariati za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika huduma ya maji kwa jamii.

Sehemu ya Msaada wa Huduma za Kiufundi

Kazi za sehemu ni:
 Kutoa msaada wa kiufundi, kifedha na kuzijengea uwezo Halmashauri za Wilaya hii ni pamoja na uundaji wa vyombo vya watumia maji, kubuni, kuandaa, kujenga na kusimamia miradi ya maji;
 Kusimamia maandalizi na utekelezaji wa miradi ya maji ya kitaifa inayosimamiwa na serikali moja kwa moja.

Sehemu ya Menejimenti na Msaada kwa Jamii
Kazi zake ni:
 Kusimamia uanzishwaji wa vyombo vya watumiaji maji kisheria ili kuwezesha usimamizi wa miradi ya maji vijijini;
 Kusaidia na kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi na wadau wengine katika utoaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira.

Sehemu ya Mipango na Utekelezaji
Kazi zake ni:

 Kusaidia na kufuatilia maandalizi ya mipango na bajeti za Halmashauri za Wilaya katika masuala ya huduma za usambazaji maji safi na usafi wa mazingira;
 Kusaidia kutoa miongozo ya utekelezaji wa mikakati ya utoaji wa huduma ya maji vijijini kwa Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Wilaya na Wadau wengine.