Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idara ya Maji Mijini

Idara inasimamiwa na Mkurugenzi na ina sehemu tatu.

Kazi zake:
 Kutoa ushauri katika uandaaji, utekelezaji na urekebishaji wa Sera na mkakati kwa masuala yanayohusu huduma ya maji kibiashara;
 Kuhamasisha maendeleo na ukuaji wa huduma ya majisafi na majitaka kibiashara kulingana na sera na mkakati;
 Kusimamia utekelezaji wa programu ya maendeleo ya huduma ya majisafi na majitaka kibiashara;
 Kutoa msaada wa kiufundi na kifedha kwa Mamlaka za Majisafi na Majitaka;
 Kusimamia utekelezaji wa shughuli za Mamlaka za majisafi na majitaka.

Idara hii pia inawajibu wa kuhakikisha kuwa huduma za majisafi na majitaka zinapatikana mijini na miji midogo hapa nchini.

Sehemu ya Kuratibu na kuwezesha Uandaaji
Kazi zake ni:
 Upitiaji, usanifu na uwezeshaji wa kifedha katika mipango ya majisafi na majitaka;
 Kutoa miongozo na kuwezesha uandaaji wa mipango ya huduma za majisafi na majitaka kwa Mamlaka za Maji;
 Inasimamia uandaaji wa mipango ya makubaliano na mikataba mbalimbali.

Sehemu ya Ufuatiliaji wa Mikataba na Ujenzi
Kazi za sehemu ni:
 Kusimamia utendaji na utoaji huduma kwa mamlaka za majisafi na majitaka;
 Inatoa miongozo na misaada ya kiufundi kwa Mamlaka za Majisafi na Majitaka, vilevile inatoa msaada katika kutekeleza na matengenezo na uendelezaji wa mifumo.

 Sehemu ya Ufuatiliaji wa Utoaji wa Huduma

Kazi za sehemu ni:
 Kusimamia utendaji na ufikishwaji wa huduma kwa mamlaka za majisafi na majitaka;
 Kutoa miongozo na misaada ya kiufundi kwa Mamlaka za Majisafi na Majitaka, ili kuwasaidia katika utendaji kazi, matengenezo na uendelezaji wa mifumo.