Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idara ya Huduma za Ubora wa Maji

 

Utangulizi.

Idara ya Huduma za Ubora wa Maji inaongozwa na Mkurugenzi na ina jukumu la  wa kutoa utaalamu na huduma zinazohusu masuala ya usimamizi wa  ubora wa maji. Idara ina mtandao wa maabara 16  nchini. Maabara hizi ziko Arusha, Bukoba, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Musoma, Singida, Shinyanga, Songea, Sumbawanga, na Tanga. Pia Idara ina kituo kimoja cha utafiti wa madini ya floraidi kilichopo Ngurdoto, Arusha.

Majukumu.

 1. Kushiriki katika kuandaa sera ya maji , kupitia viwango vya ubora wa maji, kutoa miongozo na maoni katika utekelezaji wa mikakati ya usimamizi wa ubora wa maji
 2. Kutayarisha na kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu usimamizi wa ubora wa maji.
 3. Kutoa ushauri kuhusu tafiti  mbalimbali zinazohusiana na   ubora wa maji .
 4. Kutoa ushauri wa kiufundi kwenye mitambo  ya  kusafisha maji, na  uidhinishaji wa ubora wa  madawa ya kusafisha  maji

Idara inaundwa na vitengo vitatu navyo ni :

 1. Kitengo cha uratibu  wa ubora wa maji.
 2. Kitengo cha uhakiki   na  viwango vya ubora wa maji.
 3. Kitengo cha ushauri wa  kiufundi na tafiti za ubora wa maji.

Majukumu ya vitengo hivi ni kama ifuatavyo;

a . Kitengo cha uratibuwa ubora wa maji.

 1. kushiriki katika  kutunga  Sera za ubora wa  maji, viwango, sheria  na miongozo kuhusiana na  ubora wa maji.
 2. Kuratibu na kutoa miongozo kuhusu ufuatiliaji wa ubora wa maji (ikiwa ni pamoja maji taka na utuaji anga).
 3. Kutayarisha,   kuboresha , kutunza  takwimu  za ubora wa maji na kusambaza  taarifa zake.
 4. Kutathimini na kutoa  ripoti za  viwango vya ubora wa maji
 5. Kushauri kuhusu  mipango na  utekelezaji  ya usimamizi  wa ubora wa maji.

 

b. Kitengo cha uhakiki naviwango vya ubora wa maji.

 1.  kushiriki  katika  kutunga  Sera za ubora wa maji , sheria  na miongozo kuhusiana na uhakiki  na viwango vya ubora wa maji.
 2. Kutayarisha na kupitia  miongozo  na viwango vya utendeshaji  kazi    nje na ndani  ya maabara za maji. Pia kusimamia miongozo hiyo inatekelezwa kwa usahihi.
 3. Kusimamia na kuthibiti mipango  kuhusu tathimini ya ubora wa maji.
 4. Kusimamia mchakato wa kupata ithibati kwa maabara za maji
 5. Kutoa ushauri kuhusu mapitio na uboreshaji wa viwango vya ubora wa maji na majitaka.
 6. Kutoa huduma kwa jamii na sekta binafsi kuhusiana na tathimini ya ubora wa maji na majitaka pamoja na ubora wa dawa za  kusafisha maji.
 7. Kufanya majaribio kwa  dawa zinazotumika  kusafisha  maji na kuidhinisha ubora wake.
 8. Kutoa ushauri wa kiufundi kwa viwanda kuhusu njia sahihi za  kusafisha majitaka yanayotoka  viwandani ili kuzuia uchafuzi wa vyanzo vya maji.

ix.  Kuratibu masuala ya ushahidi  wa kisheria kuhusiana na  uchafuzi wa vyanzo vya maji

(c) Kitengo cha ushauri wa  kiufundi na tafiti za ubora wa maji

 1. Kufanya tafiti na kutoa maoni katika kutayarisha Sera za ubora wa maji, viwango, sheria na miongozo.
 2. Kutoa miongozo kuhusu usimamizi shughuli za tafiti zinazofanyika na kuhakikisha matokeo yake yanasambazwa.
 3. Kutoa miongozo kuhusu uondoaji  wa masalia ya kemikali  na  madawa yaliyoisha muda wake wa matumizi.
 4. Kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya usalama  kazini  ikiwa nje na ndani ya maabara za maji.
 5. Kutoa ushauri kuhusu mchakato wa kusafisha maji, upimaji wa madawa ya kusafisha  na kuthibitisha ubora wake.
 6. Kutoa ushauri wa kitaalam kwenye mitambo ya kusafisha maji  kuhusiana na kiasi cha madawa kinachohitajika kusafisha  maji.